Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imetangaza kuwa Shirika la Ndege la Air Peace la nchini humo limejitolea kutuma ndege zake kwenda Afrika Kusini hapo kesho ili kuwasafirisha bure raia wa nchi hiyo wanaotaka kurejea nyumbani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, -Geoffrey Onyeama amesema kuwa Shirika hilo limefikia uamuzi huo baada ya kuona raia wa nchi hiyo wakishambuliwa katika vurugu hizo.
Waziri Onyeama amewataka raia wote wa Nigeria wenye ndugu na jamaa nchini Afrika Kusini kuwajulisha ili kutumia usafiri huo kurejea nyumbani.
Vurugu zimeendelea kwa siku kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini ambapo baadhi ya Raia wa nchi hiyo wamekua wakiwashambulia wageni ambao wanafanya shughuli mbalimbali nchini humo pamoja na kuharibu mali zao.