Mazishi ya pacha Anisia Bernard aliyefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili siku Nne baada ya kurejea nchini kutoka Saudia Arabia alipotenganishwa na mwenzake Melnes yanafanyika hii leo kijijini kwao Mabale wilayani Misenyi mkoani Kagera.
Tayari mwili wa Anisia umewasili wilayani Misenyi kwa ajili ya mazishi ambapo Wakazi mbalimbali wa wilaya hiyo wamepata nafasi ya kuuaga.
Watoto hao walikua wakipatiwa matibabu kwa ufadhili wa Mfalme wa Saudi Arabia katika hospitali ya Chuo Kikuu cha King Abdullah mjini Riyadh, ambapo matibabu yao yaligharimu zaidi ya Dola Laki Tano za Kimarekani.