“Nimewaita hapa ili mshuhudie kazi nzuri iliyofaywa na maafisa wa Serikali na Kikosi Kazi maalum cha kudhibiti ujangili, ninatoa huruma ya muda wa mwezi mmoja kuanzia Septemba Nne hadi Oktoba Nne mwaka huu kwa kila aliye na meno ya tembo ayasalimishe kwenye chombo chochote cha serikali, na atakayefanya hivyo ndani ya muda huo hatutamshtaki”.
Kauli hiyo ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla ameitoa jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari mara baada Kikosi kazi cha Taifa cha kudhibiti Ujangili (NTAP) kukamata watuhumiwa Wanane wa ujangili, vipande 338 na meno mazima ya tembo 75 pamoja na meno mawili ya kiboko.