Ndege ya ATCL yawasili nchini

0
304

Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), iliyokuwa ikishikiliwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini imerejea nchini baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng kuamuru ndege hiyo iruhusiwe kuondoka uwanjani hapo.

Taarifa za kuachiwa kwa ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 iliyokuwa imezuiliwa tangu tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu zimepokewa kwa shangwe na Watanzania kutoka maeneo mbalimbali.

Wananchi wengi mbali na kupokea kwa shangwe taarifa za kuachiwa kwa ndege hiyo, pia wamepongeza jitihada za serikali zilizofanikisha jambo hilo.

Ndege hiyo ya ATCL ilikua ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya mahakama hiyo ya Gauteng, baada ya raia mmoja wa nchi hiyo Hermanus
Steyn kufungua kesi katika mahakama hiyo akidai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na serikali ya Tanzania mwaka 1980.

Mahakama hiyo pia imemtaka mlalamikaji huyo Steyn kulipa gharama za kesi.