Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa taarifa rasmi ya kuachiwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama ya Guateng jijini Johannesburg.
Ngege hiyo aina ya Airbus A220-300 ilikua ikishikiliwa kwa muda wa takribani wiki Mbili na imeachiwa hii leo ambapo pia Mahakama hiyo imeamuru Mlalamikaji kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Akitoa taarifa rasmi ya serikali mbele ya Rais John Magufuli jijini Dar es salaam, Waziri Kamwelwe amesema kuwa, ndege hiyo itarejea nchini hii leo na itaendelea na ratiba zake kama kawaida.
Pamoja na taarifa hiyo Waziri Kamwelwe amesema kuwa zoezi la ununuzi wa ndege mbili kwa ajili ya kuendelea kuiimarisha ATCL linaendelea vizuri na kwamba anga la Tanzania lipo salama.