Baba Mtakatifu Francis ziarani Msumbiji

0
251

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francis, ameanza ziara yake ya siku Tatu nchini Msumbiji, ziara ambayo itamfikisha katika nchi nyingine za Afrika ambazo ni Madagascar na Mauritius.

Baba Mtakatifu Francis amekua ni Kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki Duniani kufanya ziara nchini Msumbiji, katika kipindi cha zaidi ya miaka Thelathini.

Akiwa nchini Msumbiji Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani,  anatarajiwa kulihutubia Taifa hilo ambapo anategemewa kugusia mchakato wa amani wa nchi hiyo na kuwapa pole Wananchi walioathiriwa na kimbunga mwanzoni mwa mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, – Jose Pacheco amesema kuwa, Serikali ya nchi hiyo inatarajiwa kutumia zaidi ya Dola Laki Tatu za Kimarekani kwa ajili ya ziara hiyo ya Baba Mtakatifu.

Ziara hiyo ni ya Pili kwa Baba Mtakatifu Francis Barani Afrika, tangu achaguliwe kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani mwaka  2013. m