Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya

0
113

Serikali imesema kuwa, itaendelea na jitihada zake za kuboresha huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hizo kwa ufanisi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo wakati akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Mtama, – Nape Nnauye na Mbunge wa Biharamulo,- Oscar Mukasa.

Akijibu maswali hayo kuhusu lini serikali itaboresha vituo vya afya katika majimbo hayo ya Mtama na Biharamulo,- Waziri Jafo amesema kuwa kwa sasa serikali inaendelea na mpango wake wa kuboresha vituo vya afya nchi nzima ili viweze kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Amefafanua kuwa, mbali na vituo vya afya katika majimbo hayo mawili, lakini pia kituo cha afya katika jimbo la Kigoma Kaskazini kinafanyiwa ukarabati ili kiweze kutoa huduma za afya katika mazingira bora.

Mkutano wa 16 wa Bunge unaendelea jijini Dodoma, ambapo hii leo umeingia katika siku yake ya pili.