Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu Tisa kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni kinyume cha sheria ya ubadilishaji fedha za kigeni ya mwaka 2019.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, – Muliro Jumanne amewaambia Waandishi wa Habari kuwa, watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni ya kushtukiza katika maduka na kampuni mbalimbali jijini Mwanza.
Amesema kuwa, katika operesheni hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 354 na vifaa mbalimbali vimekamatwa.