Brazil yakubali kupokea msaada

0
208

Hatimaye serikali ya Brazil imesema iko tayari kupokea misaada ya Kimataifa, kusaidia kuzima moto wa msituni unaondelea kuteketeza misitu ya Amazoni iliyoko nchini humo na inayotegemewa na mataifa katika nchi za Amerika ya Kusini.

Awali Rais Jail Barsonaro wa nchi hiyo alikataa kupokea msaada wa Dola Milioni 20 za Kimarekani kutoka kwa nchi tajiri duniani, ambazo kwa kauli moja zilikubaliana kuyasaidia mataifa ya Amerika ya Kusini kuzima moto huo unaoendelea kuwaka.

Baadhi ya Wanaharakati wa mazingira Duniani wamedai kuwa, sera mbaya za kiongozi huyo ndio chanzo cha moto huo wa msituni.