Waziri Mkuu wa Uingereza,- Borris Johnson amethibitisha kuwa ataahirisha bunge la nchi hiyo tarehe 14 mwezi Oktoba mwaka huu.
Wachunguzi wa siasa za nchi hiyo wamesema kuwa, hatua ya Johnson kuahirisha bunge ni njia mojawapo ya kuzuia mijadala kuhusiana na mpango wa nchi hiyo kujitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya, ili nchi hiyo itekeleza maamuzi yake.
Uingereza inatarajiwa kujitoa rasmi kwenye Umoja wa nchi za Ulaya mwezi Oktoba mwaka huu na kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na Umoja huo ni kwamba, nchi hiyo haipaswi kubadili tena muda huo wa kujitoa.