Bilal atimuliwa Alliance

0
561

Klabu ya Alliance FC imemtimua kocha wake Athumani Bilal, na nafasi yake kuchukuliwa na Kessy Mziray ambaye atasaidiwa na Habib Kondo pamoja na Dady Odoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, mwenendo usioridhisha wa timu hiyo hasa katika maandalizi ya msimu huu wa mashindano,  pamoja na kuanza kwa sare kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara,  ndio sababu kubwa ya kutimuliwa kwa Bilal.

Bilal ameiongoza Alliance katika michezo Saba ya maandalizi ya msimu, ambapo timu hiyo ilishinda michezo miwili na kutoka sare michezo mitano na katika mchezo wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu walitoka sare na Mbao kitendo kilichowachukiza wakuu wa timu hiyo na kuamua kumtimua.

Kibarua cha kwanza kwa kocha mpya wa klabu hiyo Kessy Mziray kitakuwa dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 14 mwaka huu kwenye dimba la Nyamagana na wakuu wa Alliance wanataka kuona timu hiyo ikicheza soka la kuvutia.