Malengo ya Tanzania TICAD7

0
274

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa, malengo ya Tanzania katika mkutano wa  Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD7) ni kuishawishi Japan kuiunga mkono Tanzania katika suala la Teknolojia na maendeleo ya viwanda ili kuiwezesha kufikia azma yake ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo baada ya kuwasili katika mji wa Yokohama nchini Japan akimwakilisha Rais John Magufuli kwa ajili ya kushiriki mkutano huo wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika utakaofanyika kuanzia Agosti 28 hadi 30 Agosti mwaka huu.