Manchester City imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, na kuwashusha Arsenal hadi katika nafasi ya Tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao Matatu kwa Moja dhidi ya AFC Bournamouth.
Mabao mawili ya Sergio Aguero katika dakika ya 15 na 64 na lile la Raheem Stearling katika dakika ya 43, yametosha kuwapa alama Tatu muhimu City kwenye uwanja wa ugenini wa Vitality na kupunguza pengo la alama na vinara Liverpool hadi kufikia alama mbili.
Tottenham Hotspurs nao wakiwa nyumbani wamenyukwa bao Moja kwa bila na Newcastle United, huku Wolverhampton Wenderers wakishindwa kutamba mbele ya Burnley na kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja.