Wanasheria wafuatilia ndege ya ATCL kushikiliwa

0
287

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ametuma ujumbe nchini Afrika Kusini kufuatilia suala la ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kushikiliwa kwa amri ya mahakama.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe amesema kuwa ana uhakika suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Ndege hiyo aina ya Airbus 220 – 300 ikiwa na abiria 83, inadaiwa kushikiliwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Thambo mjini Johannesburg kwa amri ya mahakama ya Gauteng ya nchini humo.

Katika hatua nyingine Waziri Kamwelwe amesema kuwa, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 5.3 kwa ajili ya kujenga kivuko kipya kitakachorahisisha usafiri na usafirishaji kwa Wakazi wa Mafia na Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Waziri Kamwelwe ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea eneo la Kigamboni linalotumiwa na kampuni ya Wazawa ya Songoro Marine kujenga kivuko hicho.

Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba Tani Mia Moja za mizigo na abiria Mia Mbili kwa wakati mmoja.