Kivumbi Ligi Kuu Tanzania Bara

0
170

Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imeanza kutimua vumbi Jumamosi Agosti 24, inaendelea tena hii leo kwa vilabu mbalimbali kushuka dimbani.

Katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi hiyo, timu ya Mbeya City iliwakaribisha ndugu zao Tanzania Prisons katika dimba la Sokoine, ambapo timu hizo zimetoka suluhu, wakati Mwanza Alliance FC ikilazimisha sare ya kufungana bao moja kwa moja na Mbao FC katika dimba la CCM Kirumba.

Katika michezo mingine, timu ya Namungo ambayo imepanda daraja msimu huu, ikiwa nyumbani katika dimba la Majaliwa, imeitandika Ndanda FC ya Mtwara mabao mawili kwa moja, Polisi Tanzania ambao nao wamepanda daraja msimu huu wameinyuka Coastal Union ya Tanga bao moja kwa sifuri katika dimba la Ushirika mjini Moshi.

Biashara United ya Mara ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa kumbukumbu ya CCM Karume mjini Musoma imekula kichapo cha mabao mawili kwa nunge mbele ya Kagera Sugar ya Kagera.