Majeruhi mwingine wa ajali ya moto afariki Dunia

0
233

Idadi ya watu waliofariki Dunia kutokana na lori la mafuta kupinduka na kulipuka kwa moto mkoani Morogoro Agosti 10 mwaka huu, imefikia 101.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi mwingine kufariki Dunia kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam, alikokua akipatiwa matibabu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika hospitali hiyo Aminiel Aligaesha amesema kuwa, kwa sasa wamebakiwa na majeruhi 14 kati ya 47 waliofikishwa hospitalini hapo kutoka mkoani Morogoro, na kwamba 11 wamelazwa kwenye chumba cha Wagonjwa mahututi na wengine Watatu wameanza mazoezi ya kuwawezesha kunyanyuka.