Mashabiki wakanyagana katika tamasha la muziki

0
1820

Watu walioshuhuda tukio la kukanyagana wakati wa tamasha la muziki wa kufoka(Kurap) nchini Algeria wamesema kuwa, huenda tukio hilo limesababishwa na uwanja palipofanyika tamasha hilo kujaa kupita uwezo wake.

Watu watano wamefariki Dunia na wengine zaidi ya Ishirini wamejeruhiwa katika tukio hilo na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Mashuhuda hao wamesema kuwa, tukio hilo la kukanyagana lilianza baada ya maafisa usalama kuanza kuzuia umati wa watu uliotaka kuingia ndani ya uwanja huo huku ukiwa umejaa.

Tamasha hilo la muziki lilikua likitumbuizwa na Mwanamuziki nyota wa nchi hiyo Abderraouf Derradji maarufu kama Soolking, ambaye kwa sasa anaishi nje ya Algeria, lakini amekua akiimba nyimbo zinazoelezea maisha ambayo raia wa nchi hiyo wanayapitia.

Tamasha hilo lilikua likionyeshwa moja kwa moja kupitia vituo kadhaa ya Televisheni vya nchini Algeria.