Rais Jair Bolsonaro wa Brazil amesema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na masuala ya utunzaji wa mazingira huenda yanahusika na moto mkubwa unaoendelea kuteketeza msitu wa Amazon.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Rais Bolsonaro amesema kuwa huenda mashirika hayo yanahusika na vitendo hivyo kufuatia hatua ya serikali ya Brazil kuondoa ufadhili kwa mashirika hayo.
Bolsonaro ameongeza kuwa, lengo kubwa la mashirika hayo ni kuiaminisha Jumuiya ya Kimataifa kuwa Brazil imeshindwa kuutunza msitu huo mkubwa Duniani.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti ya nchini Brazil (INPE), takribani matukio Elfu 73 moto yametokea nchini humo kati ya mwezi Januari na Agosti mwaka huu, ikilinganishwa na matukio Elfu 39,759 yaliyotokea katika kipindi kama hicho mwaka 2018.
Taarifa hiyo ya INPE imeonyesha kuwa matukio hayo yote yametokea kwenyemaeneo ya msitu wa Amazon.
Habari zaidi kutoka nchini Brazil zinasema kuwa, asilimia Sitini ya msitu huo wa Amazon ambao ni chanzo kikubwa cha mvua ipo kwenye mipaka ya Brazil na kwamba hatua ya kuharibiwa kwa msitu huo inaweza ikawa na athari kubwakwenye mabadiliko ya tabianchi Duniani.