Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amewaagiza viongozi wote wa mikoa kusimamia mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, yaliyoanza kutolewa kwenye maeneo yao.
Waziri Mhagama ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu nchini, mafunzo yanayoratibiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Amesema kuwa, serikali inaunga mkono mafunzo hayo kwa kuwa yana umuhimu mkubwa kwa vijana katika kujiimarisha kiuchumi.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye amesema kuwa, mafunzo hayo yanalengo la kutatua changamoto za maisha ndani ya jamii.