Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amethibitisha kuwa serikali yake inaendelea na mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani, mazungumzo yenye lengo la kuiomba Marekani ilegeze baadhi ya vikwazo kwa nchi hiyo.
Akizungumza na Raia wa Venezuela kupitia Televisheni ya serikali ya nchi hiyo,Maduro amesema kuwa, mazungumzo hayo yamedumu kwa miezi kadhaa sasa.
Maduro ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita wiki kadhaa baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya Venezuela, ili kushinikiza kiongozi huyo aondoke madarakani.
Kwa upande wake Rais Donald Trump wa Marekani amethibitisha kuwepo kwamazungumzo hayo, bila kutaja ni maafisa gani wanaohusika, lakini amesisitizakuwa ni wa ngazi ya juu.
Marekani ni moja ya Mataifa zaidi Hamsini ambayo hayamtambui Maduro kama Rais wa Venezuela.