The Rock afunga ndoa ya siri

0
1810

Muigizaji maarufu wa filamu Duniani Dwayne Johnson maarufu kwa jina la The Rock, amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Lauren Hashian.

The Rock mwenye umri wa miaka 47 na Raia wa Marekani, amebahatika kupata watoto wawili na Lauren kabla ya ndoa yao.

Sherehe ya harusi ya Dwayne na Lauren imefanyika kwa siri katika visiwa vya Hawaii, mahali ambapo The Rock amekulia.