Zaidi ya Wafanyabishara Elfu Sitini wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo – DRC ambao wamekua wakivuka mpaka na kuingia katika nchi za Rwanda na Uganda mara kwa mara wanatarajiwa kupatiwa chanjo dhidi ya Ebola, ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Takwimu za hivi karibuni za watu wanaougua Ebola katika mji wa Goma, ambao una shughuli nyingi za kiashara na unaopakana na Rwanda, zimeongeza wasiwasi huenda wakaingiza ugonjwa huo nchini humo.
Kitengo cha kukabiliana na ugonjw wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo takribani watu Elfu Moja na Mia Tisa wamefarinki Dunia baada ya kuugua ugonjwa huo kimesema kuwa, Maafisa wa Afya nchini Rwanda nayo imeagiza Dozi Laki Moja za chanjo ili iweze kutoa chanjo kwa Wafanyabiashara wake.
Hata hivyo haijafahamika chanjo hiyo itaanza kutolewa lini.