Rais wa Shelisheli atua Tanzania kushiriki mkutano wa SADC

0
401
Rais wa Shelisheli, Danny Faure (kushoto) akipokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo kwa ajili ya Mkutano wA 39 wa SADC unaotarajia kuanza kesho.

Rais wa Shelisheli, Danny Faure amewasilini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam nchini Tanzania.

Rais Faure amewasili leo Ijumaa Agosti 16, 2019 saa 2:18 asubuhi na kupokewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Innocent Bashungwa.

Kiongozi huyo wa visiwa hivyo amekwenda Tanzania kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kesho Agosti 17 na 18, 2019.

Faure ni Rais wa pili kuwasili Tanzania akitanguliwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ambaye aliwasili juzi Jumatano Agosti 14,2019 kwa ziara ya siku mbili ya jana na leo kisha kesho atashiriki mkutano huo wa SADC.