JESHI LA POLISI LAAHIDI KUIMARISHA ULINZI WAKATI WOTE WA MKUTANO WA SADC.

0
324
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na namna Jeshi lake lilivyojipanga kuimarisha ulinzi wakati wote wa Mkutano wa 39 wa SADC

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linatarajia kupokea wakuu wa nchi kuanzi tarehe 16.08.2019.


Ulinzi utaimarishwa kuanzia mapokezi yao Airport, Hoteli wanazofikia na kuelekea katika kumbi za mikutano.

Aidha tutaimarisha ulinzi na vikosi vyote vya doria mbwa, farasi na helicopter ili kuhakikisha mkutano unamalizika salama.

Sambamba na hilo tunaendelea Kukamata pikipiki zote na magari yanayovunja sheria na katazo la kuingia mjini ambapo jumla ya magari na pikipiki ni 126 ambayo yamechukuliwa hatua za kisheria.

Madereva wengi wameendelea kutupa ushirikiano katika siku zote za mkutano huu wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara SADC.

Wananchi wawe watulivu wakati misafara ya viongozi ikipata maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.