SERIKALI YA TANZANIA YAWAPONGEZA WAANDISHI WANARIPOTI MKUTANO YA SADC

0
273
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk.Hassan Abbasi .


Serikali imesema inafurahishwa na kazi nzuri na ya kizalendo inayofanywa na waandishi wa habari nchini Tanzania ambao wanaandika habari za mikutano ya Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrikka (SADC) na kuomba waendelee hivyo hivyo kwani sasa mikutano hiyo ndio imeanza kupamba moto.

Hayo yamesemwa leo Agosti 13,mwaka huu wa 2019 na Msemaji Mkuu wa Serkali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dk.Hassan Abbasi wakati anazungumza na waandishi wa habari wanaoandika habari za SADC katika mikutano inayoendelea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kuhusu namna ambavyo waandishi wa habari wanaandika habari za jumuiya hiyo Dk.Abbasi amesema Serikali kila siku inaangalia, inatazama na inaona,hivyo imefurahishwa na kazi kubwa na nzuri ya kizalendo na kihistoria inayofanywa na waandishi wa habari na hakika wanastahili pongezi.

“Waandishi wa habari naomba nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwenu na vyombo vyenu vya habari,mnaandika habari za SADC kwa weledi mkubwa na uliojaa uzalendo kwa nchi yetu. Tunafuatilia kila siku na ninakilasabababu ya kuwaambia hadi sasa Serikali tunaridhishwa na habari mnazoandika.Kwa mujibu wa ratiba sasa ndio kasi imepamba moto kwani tuko katikati kuelekea kwenye mkutano wenyewe wa 39 wa SADC.

” Kama kuna kitu natamani ni kuona waandishi wa habari mnaendelea kuandika kwa uzalendo.Tutafurahi kama tutamaliza kama ambavyo tumeanza.Naamini kwenye uandishi wa habari unaowajibika kwa misingi ya taaluma ya habari,na mara zote kwenye mikutano yangu nimekuwa nikisisitiza hilo.Tuendelee kuandika habari kwa misingi ya uwajibikaji wenye weledi,”amesema Dk.Abbasi.


M

Alipoulizwa kuhusu faida ambayo nchi ya Tanzania inaipata kutokana na vikao vinavyoendelea vya Jumuiya hiyo, Dk.Abbasi amejibu kuna faida nyingi endelevu ambazo zimeanza kupatikana na zitaendelea kupatikana.

Amefafanua kuna faida ambazo zinaonekana moja kwa moja na zipo faida ambazo kila Mtanzania kwa nafasi yake anaziona na faida za jumla kwa nchi yetu.”Kwenye wiki ya viwanda washiriki walipata nafasi ya kutembelea baadhi ya viwanda.

“Wamekiri na kuridhishwa na teknolojia ya hali ya juu ambayo wameiona kwenye viwanda vyetu.Ni matarajio wetu washiriki hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuielezea Tanzania yetu kwenye nchi zao na haswa tulivyojiimarisha katika eneo la viwanda.Hii faida kubwa kwa nchi yetu,”amesema.

Alipoulizwa kuhusu uhifadhi wa picha na historia ya Jumuiya ya SADC ,Dk.Abasi amejibu Tanzania inao utaratibu mzuri wa kuhifadhi picha,sauti na picha za video zinazohusu ukombozi wa Bara la Afrika na kufafanua uhifadhi huo unafanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Pia amesema Tanzania ni mwenyeji wa mradi wa kuhifadhi historia ya ukombozi wa Bara la Afrika na makao makuu ya.mradi huo yapo hapa hapa nchini, huku akishauri Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo ambayo historia ya bara la Afrika imehifadhiwa.