20 kuwania taji la Miss Tanzania

0
2445

Walimbwende 20 Agosti Nane mwaka huu watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Tanzania ambalo pia ni tiketi ya kushiriki mashindano ya urembo ya dunia, Miss World.

Mlezi wa warembo hao Fatma Mtisiri amesema kuwa fainali za Miss Tanzania kwa mwaka huu zitakuwa na upinzani mkubwa.

Sammy Cool ni mwalimu wa muziki wa warembo hao wanaowania taji la Miss Tanzania kwa mwaka huu ambaye amesema kuwa warembo wa mwaka huu wana tofauti kubwa na aliowahi kuwafundisha miaka ya nyuma kwa kuwa wana ari ya kujifunza.

Naye Miss Tanzania kwa mwaka 1997, Saida Kessy amesema kuwa maandalizi mazuri waliyoyapata warembo hao yataleta mchuano mkali kati yao.

Kabla ya fainali hizo, washiriki wa shindano hilo la Miss Tanzania wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii.