Waziri Mkuu KASSIMU MAJALIWA ameuagiza uongozi wa mkoa wa MOROGORO kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu kujenga uzio na mnara wa kumbukumbu katika makaburi ya KOLLA utakaotambulisha eneo ilikozikwa miili ya watu waliopata ajali ya kuungua moto na kuteketea baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la MSAVU manispaa ya MOROGORO.
Akizungumza katika ibada ya mazishi ya mmoja kati ya miili 60 iliyozikwa katika makaburi ya KOLA, Waziri Mkuu MAJALIWA amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kunakuwepo na kumbukumbu ya ajali hiyo iliyopoteza maisha ya watu wengi.