Watu 11 wamethibitika kufa katika ajali iliyohusisha magari matano yaliyokuwa yameongozana katika mteremko wa mlima wa Igawilo jijini Mbeya ambayo yamegongwa na gari jingine kubwa.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Urich Matei amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori aina ya Scania kushindwa kulimudu gari hilo ambalo lilikuwa na matatizo katika mfumo wa breki.
Kufuatia ajali hiyo Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa za watu wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo.