Dkt Shein Afurahishwa na bidhaa za ngozi za kiwanda cha Karanga

0
248
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Dkt Ali Mohamed Shein akimsikiliza Afisa Masoko na Uhusiano wa Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Ngozi cha Mkoani Kilimanjaro Fredrick Njoka kuhusina na Ubora wa bidhaa za kiwanda hicho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Dkt. Ali Moamed Shein amewataka watanzania na Taasisi za ulinzi nchini kutumi bidhaa bora za ngozi zinzozalishwa na kiwanda cha Karanga Leather Industry cha Mkoani Klmanjaro.

Dkt Shein ametoa rai hiyo wakati alipofanya ziara kwenye Banda la Kiwanda hicho kwenye maonesho ya 4 ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika –SADC yaliyomalizika hii leo Jijini Dar es salaam.

Rais Shein amesema bidhaa zinzozalishwa na kiwanda hicho zimeonekana kuwa bora na hivyo kuwataka watanzania na taasisi za ulinzi kuzitumia bidhaa hizo kwa lengo la kuinua bidhaa za Tanzania.

Ameongeza kuwa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngoz cha Karanga kimekuwa mfano kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora na hivyo n lazma watanzania waking mkono.

Kwa upande wake Afisa Masoko na Uhusiano wa kiwanda hicho Fredrick Njoka amemueleza Rais Shen kuwa bidhaa zote wanzozizalisha wanatumia malighafi za hapa nchini.