TEITI Kuweka wazi mikataba ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia

0
291
Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika Sekta Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Bwana Erick Ketagory, akimweleza jambo Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt Hassan Abass aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Maonesho ya 4 ya Viwanda ya Jumuiya ya SADC

Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika Sekta Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Erick Ketagory, amemwelezea Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abass kuwa TEITI ipo kwenye hatua za awali za maandalizi ya ripoti za TEITI kwa mwaka wa fedha 2016/17 na 2017/18.

Aidha, amesema kuwa,TEITI imejiandaa kutekeleza takwa la sheria ya TEITA,2015 ya uwekaji wazi wa mikataba ya kampuni za Madini,Mafuta na Gesi Asilia Tanzania.

Bwana Ketagory ametoa taarifa hiyo kwenye maonesho ya 4 ya Viwanda ya SADC ambayo yanafikia tamati siku ya leo August 8,2019 katika viwanja vya JNICC Jijini Dar es salaam