Waziri Mkuu Majaliwa aweka mkazo fursa za kuwekeza nchini Tanzania

0
1223

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewashauri watanzania wenye nia ya kuwekeza hapa nchini kwa ajili ya soko la ndani la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika –SADC kutumia fursa ya maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC kutafuta wawekezaji wa nchi hizo ambao wanaweza kuingia ubia.

Waziri Mkuu MAJALIWA amesema hayo jijini DSM wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya walioshiriki maonesho ya NNE ya wiki ya viwanda ya SADC.

Katika mabanda hayo yakiwemo ya taasisi za serikali, sekta binafsi, makampuni, wajasiriamali na yale ya kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa afrika SADC. Yametembelewa na waziri mkuu KASSIM MAJALIWA ili kujionea ubunifu na utayari wao wa kuzalisha bidhaa zilizo bora kwaajili ya soko la SADC.

Amesisitiza kuwa maonesho hayo ya viwanda ni fursa ya kuingia ubia na wawekezaji wa nchi wanachama ili kutekeleza kwa vitendo sera ya viwanda.