CRDB yapata faida ya Shilingi Bilioni 61

0
1158
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akisisiza jambo wakati wa mkutano wa kutoa taarifa ya Robo ya pili ya utendaji kazi wa benki hiyo

Benki ya CRDB imepata faida ya  shilingi bilioni 61 katika robo ya pili ya mwaka 2019,ambayo ni zaidi ya faida waliyopata kwa mwaka mzima 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema ongezeko hilo  linatokana na benki hiyo kuwekeza katika miradi ya kilimo na ile ya maendeleo na hivyo wateja wake kuendelea kuimini zaidi.

Aidha Nsekela amesema Matumizi ya kibenki kwa kutumia miamala ya kimitandao ya simu imeongezeka kwa asilimia 80 hapa nchini kufuatia kuimarika kwa huduma hizo katika baadhi ya makampuni ya simu.

Gloria Michael/James Range