Waziri wa Maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangalla amesema mkutano wa SADC ni fursa ya kukuza sekta ya utalii, pamoja na watoa huduma kutoa huduma bora ili kukuza sekta hiyo. Akizungumza Jijini Dsm Waziri Kigwangalla amesema kuwa watoa huduma hawana budi kutoa huduma bora zitakazokidhi mahitaji na hivyo kuweza kupanua wigo wa fursa zitokanazo na utalii wa mikutano.
Nao Baadhi ya watoa huduma za malazi na chakula Jijni Dar es salaam wamesema kuwa ujio wa wageni wa SADC umekua na manufaa kwao na kusema wamejiandaa kutoa huduma bora zitakazofanya wageni hao kutaka kurejea tena hapa nchini.
Gloria Michael/James Range