Korea Kaskazini yafanya jaribio lingine la Makombora yake

0
163
Makombora ya Majaribio ya Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imeripotiwa kufanya jaribio lingine la kurusha makombora, ikiwa ni mara ya nne katika kipindi cha wiki mbili.

Taarifa za Korea kaskazini  kurusha makombora hayo kwa majaribio, zimetolewa na jeshi la Korea Kusini ambapo taarifa hizo zinasema majaribio hayo yamefanyika katika pwani ya jimbo la HWANGHAE KUSINI.

Korea kaskazini imefanya majaribio hayo, wakati majeshi ya MAREKANI na KOREA KUSINI yakiwa katika zoezi la pamoja la kivita lililoanza jana.