Rais wa zamani wa MAREKANI BARACK OBAMA ametoa wito kwa raia wa marekani kukataa kabisa matamshi yanayoashiria chuki na ubaguzi yanayotolewa na baadhi ya viongozi nchini humo.
OBAMA amewasisitizia wamarekani kupaza sauti na kuzitambua haki zao, kwa sababu hakuna sheria inayoruhusu viongozi kuwatamkia maneno yanayowasababishia woga, na uhasama pamoja na vitendo vya unyanyasaji kwa wahamiaji ambapo wanaonekana hawapaswi kuishi nchini humo.
Katika kauli hiyo ya OBAMA hakutaja jina la kiongozi anayemshtumu kuhusika na matamshi ya chuki na ubaguzi, na kuongeza kuwa watu wa wamrekani wanapaswa kuheshimiana kwa kuwa ni taifa moja lenye jamii mchanganyiko.
Story by. Vumilia Mwasha/ James Range