Mawaziri wa Afya wa DRC na Rwanda kukutana kujadili namna ya Kutokomeza Ebola

0
128

Mawaziri wa afya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya KONGO na RWANDA leo wanakutana kujadili na kuandika pendekezo litakalowasilishwa katika shirika la Afya Duniani WHO juu ya kukabiliana na ugonjwa wa EBOLA.

Mawaziri hao wanakutana nchini RWANDA ambapo wizara ya afya nchini DRC imesema Ugonjwa wa Ebola unaweza kuendelea kuwepo nchini huko kwa zaidi ya miaka mitatu ijayo kutokana na baadhi ya watu kushindwa kujitokeza katika vituo vya afya mara wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Tayari Nchi hizo zimeimarisha hatua muhimu za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo katika maeneo ya mpaka wa DRC na RWANDA ikiwa ni pamoja na kuosha mikono kwa maji mengi kabla ya kusalimiana na watu wa upande mwingine wa mpaka wa nchi hizo.