Watu wanne wamejeruhiwa katika ajali ya ndege ndogo ya kampuni ya tropical inayofanya safari zake kati ya Mafia na Dar es salaam
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Mafia SHAIBU NDUNDUMA ajali hiyo imetokea majira ya saa 4:30 asubuhi ya leo baada ya ndege hiyo kuanguka ilipokuwa inaruka katika uwanja wa ndege wilayani Mafia
Jumla ya abiria 9 walikuwemo katika ndege hiyo na rubani mmoja, ambapo wanne waliojeruhiwa ni abiria pekee.
Majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea na matibabu katika hospitali wilayani Mafia na mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika
Story by. Vumilia Mwasha