Ujenzi wa Miradi ya Umeme na Upanuzi wa Bandari Utachochea Ukuaji wa Viwanda:Waziri Bashungwa

0
235

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema kasi ya Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Bonde la Mto Rufiji na Upanuzi wa Bandari ya Tanga, Mtwara na Bandari ya Dar es Salaam utasaidia ukuaji wa Viwanda hapa nchini.

Akisoma taarifa ya wizara yake wakati wa hafla ya ufunguzi  wa maonesho ya 4 Viwanda ya Jumuiya ya SADC Waziri Bashungwa amesema, kasi ya ujenzi wa miundombinu hiyo ni kiashiria tosha kuwa ukuaji wa viwanda utakuwa na manufaa makubwa hapa nchini.

Waziri Bashungwa amesema, sekta ya viwanda inayoendelea kukua kwa kasi hapa nchini itapata nguvu zaidi baada ya miradi hiyo kukamilika na hivyo kurahisiha uzalishaji wa bidhaa za viwanda na kuzisafirisha hata nje ya nchi.

Waziri Bashungwa amesema kukamilika kwa mpango wa kufanya biashara “Blue Print” utaondosha vikwazo vingi vilivyokuwa vikichelewesha ukuaji wa biashara na uzalisha nchini Tanzania.