Nadir Haroub Canavaro: Wachezaji wakongwe wanaumuhimu mkubwa kwenye timu ya Taifa.

0
374

Meneja wa timu ya Taifa (Taifa Stars,Nadir Haroub Canavaro amesema wachezaji wakongwe wanaumuhimu mkubwa kwenye timu ya Taifa.

Akiongea na TBC Jijini Nairobi iliko timu ya Taifa Canavaro amesema wachezaji wakongwe wamekuwa viongozi wazuri ndani ya dimba na nje ya dimba na wanawaongoza vizuri wachezaji vijana.

Baadhi ya wachezaji wakongwe kwenye timu ya Taifa ni kipa Juma Kaseja, Kelvin Yondani na Erasto Nyoni ambao ni nguzo kubwa ya Taifa Stars kwenye michezo mbalimbali.

Taifa Stars kesho itacheza mchezo wa marudiano wa kufuzu kwa michuano ya CHAN dhidi ya Kenya ambao inalazimika kushinda au kutoka sare ya magoli ili iweze kusonga mbele.