SIMBA DAY ITAKUWA SIKU YA KIPEKEE MWAKA HUU-AUSSEMS

0
117

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji Patrick Aussems amesema Siku maalumu ya Simba(Simba Day) mwaka huu itakuwa ya kipekee kulinganisha na miaka ya nyuma kutokana na aina ya wachezaji wanaounda kikosi hicho.

Akizungumza na Mtandao wa Simba kutokea nchini Afrika ya Kusini Kocha huyo Raia wa Ubelgiji amesema kwa sasa wanajiandaa kurejea nchini na jambo kubwa wanalolitazamia kwa sasa ni mchezo wa siku hiyo dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Simba wamekamilisha program yao ya mazoezi nchini Afrika Kusini kwa kutoka Sare ya kufungana Bao moja kwa moja na Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini.

Baada ya Simba day Mabingwa hao wa Tanzania wanatarajiwa kushuka Dimbani ugenini kuanza hatua ya awali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Dhidi ya mabingwa wa Msumbiji UD Songo.

Hata hivyo Kocha Aussems amewatakamashabiki wa Simba kuujaza uwanja wa taifa kama kawaida yao ili kuwaongezea nguvu kwa kila hatua wanayocheza kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa ya Afrika msimu huu.