Boko Haram Yashambulia Watu

0
264

Watu sitini na tano wameuawa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram kuwashambulia watu waliokuwa katika msiba huko Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Akizungumzia tukio hilo, kiongozi wa Serikali katika jimbo la Borno, Muhammed Bulama amesema wapiganaji hao wa Boko Haram waliwavamia watu waliokuwa katika shughuli ya msiba na kuanza kuwashambulia kwa risasi na kusababisha vifo hivyo.

Ameongeza kuwa shambulio hilo huenda ni sehemu ya Kundi hilo la Boko Haram kulipa kisasi baada ya wananchi katika kijiji kimoja kuwauwa na kuwanyang’anya silaha kumi wapiganaji kumi na mmoja wa kundi hilo, baada ya konekana katika kijiji hicho.

Kufutia shambulio hilo la Msibani, Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amelilaani na kuliagiza jeshi la nchi hiyo kufanya Doria ya angani na ardhini ili kuwabaini na kuwakamata wapiganaji hao wa Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya shambulio kadhaa dhidi ya wananchi wa Nigeria na kusababisha vifo.