Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Dkt. DAMAS NDUMBARO amewasihi watanzania hasa vijana kulinda na kujifunza historia ya taifa ikiwemo uhusiano wa TANZANIA na nchi nyingine.
Naibu waziri Dkt. NDUMBARO amesema hayo alipotembelea maeneo mbalimbali waliyoishi waasisi wa harakati za ukombozi wa nchi zilizo Kusini mwa AFRIKA jijini DSM.