Joto lazidi kupanda Barani ulaya

0
452

Hali ya joto katika baadhi ya mataifa barani Ulaya inaripotiwa kupanda zaidi na kuvunja rekodi ya viwango vya juu vya hali ya joto vilivyowahi kurekodiwa katika baadhi ya mataifa hayo.

Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinaarifu kuwa hali ya joto imerekodiwa kufikia nyuzi joto 42.6c, ambapo nchini Ujerumani kiwango cha hali ya joto kimerekodiwa kufikia nyuzi joto 41.5c  na Uholanzi kiwango cha hali ya Joto kimefikia nyuzi joto 40.7C.

Hata hivyo taarifa za mamlaka za utabiri wa hali ya hewa katika mataifa hayo zinasema kuwa hali hiyo ya kiwango cha joto inaweza kuongezeka ambapo nchini Ufaransa kiwango hicho kinaweza kufikia nyuzi joto 43 katika baadhi ya maeneo nchini humo.