Serikali nchini Marekani inatarajia kurejesha utekelezaji wa adhabu ya kifo, baada ya kusitishwa kwa adhabu hiyo kwa miaka kumi na sita.
Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa utekelezaji wa adhabu hiyo ya kifo inatarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu na mwezi Januari 2020 kwa wahalifu waliohukumiwa adhabu hiyo kwa makosa ya mauaji na ubakaji wa watoto na wazee.
Akizungumzia hatua ya kurejeshwa kwa adhabu hiyo ambayo imekuwa ikipingwa na baadhi ya wanaharakati na wanasiasa mbalimbali nchini humo, Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr amesema adhabu hiyo itawahusu wahalifu hatari na sugu.
Amesema katika kipindi hicho cha mwezi Disemba mwaka huu na Januari mwaka 2019, adhabu hiyo itatekelezwa kwa wahalifu watano.