Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Shirika la viwango Tanzania TBS kufika mara moja katika kiwanda cha Plasco na kuweza kufanya mazungumzo ya namna gani ataweza kuwapa ithibati ya bidhaa zao kukubalika na kupata soko kiurahisi ndani na nje ya nchi
Waziri amebainisha hayo leo Julai 24 alipozindua kiwanda kinachotumia teknolojia mpya ya utengenezaji wa makaravati kwa kutumia plasitiki badala ya zege na kuwataka watendaji wote waliochini ya wizara yake kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji