Rais Magufuli apokea kilo 35 ya dhahabu iliyoibiwa nchini Tanzania

0
336

Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amepokea kilo 35.267 za dhahabu pamoja na fedha taslim zilizokuwa zimetoroshwa hapa nchini na kukamatwa nchini KENYA.

Rais MAGUFULI amepokea dhahabu hiyo iliyokamatwa mwezi Februari mwaka 2018 pamoja na fedha zilizokamatwa mwaka 2004 Ikulu jijini DSM kutoka kwa ujumbe maalum wa Rais UHURU KENYATTA wa KENYA ikiwa ni matunda ya mazungumzo waliyofanywa wilayani CHATO hivi karibuni.

Vita dhidi ya uhujumu wa rasilimali za Taifa vimeendelea kushika kasi chini ya awamu ya tano baada ya dhahabu zilizotoroshwa nchini mwaka jana na kukamatwa nchini KENYA pamoja na fedha zilizoibwa mkoani KILIMANJARO mwaka 2004 kurejeshwa na kukabidhiwa kwa rais na maafisa wa serikali ya KENYA