CCM yamteua Mtaturu kuwania ubunge wa singida mashariki

0
341

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imemteua Miraji Mtaturu kuwania ubunge wa jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya chama hicho.

Mtaturu ameteuliwa kuwania jimbo hilo katika kikao kilichofanyika hii leo jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Rais Dkt. John Magufuli.

Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuteua mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Singida Mashariki.

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Mashariki umepangwa kufanyika Julai 31 mwaka huu baada ya Spika wa bunge kutangaza jimbo hilo kuwa wazi na baadae Tume ya Taifa ya Uchaguzi- NEC kutangaza ratiba ya uchaguzi katika jimbo hilo.