Rais John Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kufanya kazi kwa weledi na askari atakayeshindwa kusimamia kanuni za jeshi hili achukuliwe hatua kali
Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa nyumba za makazi ya serikali polisi mkoani Geita ambapo katika taarifa yake Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amebainisha kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu zaidi ya askari 54 wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali
Serikali imetoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mia nne kwa ajili ya makazi ya askari wa jeshi la polisi nchini ambapo hadi sasa ni nyumba 114 zimekwisha kamilika.