Meneja na Mhasibu mradi wa maji kukamatwa

0
411

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameamuru kukamatwa kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Heru Juu wilayani Kasulu mkoani Kigoma  na Mhasibu wake kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na kutotunza kumbukumbu za mapato ya mradi huo.

Naibu Waziri Aweso aliyeko ziarani mkoani Kigoma ametoa agizo hilo kufuatia taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kubaini upotevu wa zaidi ya shilingi Milioni 15 zilizokusanywa katika mauzo ya maji.