Rais John Magufuli apokea tuzo za mlima Kilimanjaro na hifadhi ya Serengeti

0
411

Rais MAGUFULI amekabidhiwa tuzo mbili ambazo TANZANIA imekabidhiwa hivi karibuni ikiwa ni tuzo ya kuongoza kuwa na mbuga nzuri ya SERENGETI na kuwa na Mlima bora barani AFRIKA wa KILIMANJARO.

Halikadhalika amekabidhiwa zawadi ya sanamu ya taswira ya Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE ambaye alilinda rasiliamali za Taifa.

Aidha Rais Dkt. MAGUFULI  ametoa  pole kwa wanahabari nchini  kwa kupoteza  wenzao watano waliofariki dunia katika ajali ya barabarani wakiwa safarini kwenda mkoani GEITA katika uzinduzi huo wa hifadhi ya BURIGI na kusema kuondoka kwa vijana hao ni pigo katika tasnia ya habari.